Aisee DSTV!

Aishi Manula amalizana na Simba SC, afuata nyayo za John Bocco

Mlindalango namba moja nchini Tanzania, Aishi Manula ameamua kuongeza kandarasi ya kuendelea kuitumikia miamba ya soka nchini Simba SC.

Manula ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa nchini na wawakilishi wa Taifa, ambao wanatarajia kushiriki tena michuano mbalimbali ya kimataifa. Huyu ni mchezaji wa pili ndani ya wiki hii kuongeza mkataba baada ya hapo juzi kushuhudia John Bocco akiongeza kandarasi

Kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagram, Simba imeaanika makubaliano yaliyofanywa kati ya uongozi na nyota huyo mwenye mafanikio makubwa tangu kujiunga na timu hiyo.

“Tanzania one, kipa namba moja wa nchi Aishi Salum Manula ameongeza mkataba mpya wa miaka mitatu na mabingwa wa nchi Simba SC. Sasa ni rasmi Manula ataendelea kuwa nasi mpaka Juni 2022.” #NguvuMoja

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW