Habari

Ajabu: Madaktari watoa penseli ndani ya kichwa cha mwanaume baada ya kuishi nayo kwa miaka 15 bila kugundua

Katika hali ya kustaajabisha mwanaume mmoja mwenye miaka 24 ametolewa penseli ya kuandikia/kuchorea iliyokuwa ndani ya fuvu la kichwa chake kwa miaka 15 bila kugundua. Hebu vuta taswira, ile penseli inayotumiwa na watoto wadogo mashuleni, imekaa ndani ya kichwa cha mtu kwa miaka 15!

penseli

Ni jambo la kushangaza right? Inaaminika kuwa mwanaume huyo aliwahi kupata ajali udogoni iliyopelekea penseli hiyo kuingia kichwani kwake na kukuwa nayo mpaka alipokuja kufanyiwa uchunguzi na madaktari miaka 15 baadaye.

Baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa, baridi, na kutokuona vizuri kwa jicho moja mwanaume huyo raia wa Afghanistan ambaye hajatajwa jina, aliamua kwenda hospitali kuchunguza afya yake na penseli hiyo ilionekana katika scan aliyofanyiwa 2011.

Baada ya hospitali ya’ The Aachen University Hospital’ ya Ujerumani kumfanyia uchunguzi, ilitoa ripoti kuwa wamekuta peseli ya cm 10 katika fuvu la kichwa chake ambayo pia ilikuwa imeliumiza jicho lake la kulia.

Baada ya kugundulika kwa tatizo hilo madaktari hao walifanikiwa kuiondoa penseli katika kichwa chake, na kumpa matibabu ya matatizo aliyokutwa nayo na ripoti inasema hakukua na madhara makubwa baada ya matibabu hayo.

Msemaji wa hospitali hiyo Mathias Brandstaedter amesema taarifa kuhusiana na tatizo la mwanaume huyo imetoka hadharani hivi karibuni baada ya kuwasilishwa katika mkutano wa madaktari.

Source: CBS NEWS

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents