Habari

Ajali ya ndege ya jeshi yaua watu 257

Watu wapatao 257 wamefariki dunia kwenye ajali ya ndege ya jeshi huko nchini Algeria usiku wa kuamkia leo Aprili 11, 2018.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la AP limeeleza kuwa ndege hiyo imeanguka muda mfupi baada ya kutoka katika kambi ya Boufarik iliyopo nje ya mji wa Algiers na ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Bechar .

Jeshi la anga nchini Algeria limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limesema ndege hiyo ni aina ya Ilyusin II-76 na ilikuwa imebeba baadhi ya askari wa jeshi hilo.

Ajali za kuanguka kwa ndege za jeshi nchini Algeria yamekuwa yakiongezeka kwa kasi mbapo tangu mwaka 2010 hadi mwaka 2018 zaidi ya matukio makubwa matatu yanayohusisha ajali za ndege yametokea nchini humo.

Ambapo mwaka 2012 ndege mbili za jeshi zililipotiwa kugongana nchini humo wakati wanajeshi wakifanya mazoezi na mwaka 2014 zaidi ya wanajeshi 70 walipoteza maisha kwenye ajali nyingine ya ndege ya jeshi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents