Habari

Ajali ya Ndege yaua watu 15, Rubani atoka salama (+video)

Watu 15 wamefariki dunia papo hapo huku Rubani akinusurika, baada ya Ndege ya mizigo aina ya Boeing 707 mali ya jeshi la Iran kuanguka nje kidogo ya mji mkuu wa Iran, Tehran .

Waokoaji wakiwa katika eneo la ajali na vyombo vya usalama vikifanya kazi pamoja baada ya ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 707 kuanguka uwanja wa ndege wa Fath magharibi mwa Tehran, Iran, Jumatatu, Jan. 14, 2019.
Waokoaji wakiwa katika eneo la ajali na vyombo vya usalama vikifanya kazi pamoja baada ya ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 707 kuanguka uwanja wa ndege wa Fath magharibi mwa Tehran, Iran, Jumatatu, Jan. 14, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Iran, Ndege hiyo ilikuwa imebeba nyama kutoka Kyrgyzstan imeanguka jana Jumatatu ilipokuwa inajaribu kutua magharibi mwa mji mkuu wa Iran, Tehran.

Saha Airlines Boeing 707-3J9C plane crash - Tehran, Iran

Ndege hiyo, ambayo ina fanya shughuli za kiraia, ilikuwa inajaribu kutuwa katika hali ya dharura majira ya saa mbili na nusu asubuhi, Jumatatu, katika uwanja wa ndege wa Fath, uwanja ambao uko chini ya mamlaka ya majeshi ya Revolutionary Guard. Ndege hiyo ilitoka nje ya njia yake wakati inatua, na kugonga uzio na kuingia katika makazi ya watu.

Shirika la habari la AP limeripoti kuwa ajali hiyo ya ndege imeshuhudia janga lingine la hivi karibuni la usafiri wa anga, ambapo ilikuwa na matumaini ya kubadilisha ndege zake kongwe kwa kununua mpya chini ya masharti ya makubaliano ya nyuklia ya 2015 baina yake na mataifa yenye nguvu duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents