Uncategorized

Akaunti rasmi za Facebook na Twitter za rais Uhuru Kenyatta zafutwa, yadaiwa ujumbe tata uliyoandikwa asubuhi ya leo ndiyo chanzo

Akaunti zote rasmi za mitandao ya kijamiii ya rais wa Kenya Uhuru Kenyata zimefungwa baada ya kutumiwa na watu ambao ”hawajaidhinishwa”, amesema mkuu wa wafanyakazi wake kwenye ujumbe wa Twitter.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Nzioka Waita hakutoa taarifa kuhusu namna ya uingiliwaji wa mitandao hiyo ulivyotokea, lakini akaongeza kuwa itarejeshwa tena mtandaoni baada ya kuchukuliwa kwa “hatua za suluhu ya tatizo hilo,”

Akaunti za Twitter na Facebook za Bwana Kenyatta zina mamilioni ya wafuasi.

Gazeti la kibinafsi la The Star nchini humo limeripoti kuwa ujumbe uliotumwa kwenye Twitter unaoangaliwa kama kuwa wenye utata wa kisiasa, uliotumwa leo asubuhi, ulikuwa ndio sababu ya kufungwa kwa akaunti hizo.

Gazeti la The Star lilishirikisha umma picha ya ujumbe huo wa Twitter:

Ujumbe wa Twitter unaoangaliwa kama sababu ya kufungwa kwa akaunti za Twitter na Facebook za rais Kenyatta, kulingana na gazeti la The Star

Gazeti hilo limeripoti kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye ujumbe huo tata yaliyosema “mshirika wangu wa karibu wa kisiasa” katika twittee hiyo huenda ulimaanisha Naibu rais wa Kenyatta, William Ruto.

Wafuasi wa Bwana Ruto wamekuwa wakikosoa vikali vita vya rais Kenyatta vya hivi karibuni dhidi ya ufisadi ambavyo vimesababisha kukamatwa na kuhojiwa kwa maafisa wa serikali, wakisema kuwa vimekuwa na njama dhidi ya naibu wake.

Wanasema kuwa watu walio karibu na Bwana William Ruto wamekuwa wakilengwa.

Rais Uhuru Kenyatta na Bwana Odinga

Uhusiano wa karibu wa hivi karibuni wa rais Kenyatta na Bwana Odinga aliyekuwa mpinzani wake unaonekana kama njama za kuweka kando kisiasa naibu rais William Ruto

Uhusiano baina ya viongozi hao wawili , ambao waligombea nafasi zao chini ya Muuungao wa Jubelee, katika uchaguzi wa mwaka 2013 na 2017, unasemekana kuingia dosari hivi karibuni, husasn baada ya Bwana Kenyatta kusaini makubaliano na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Bwana Odinga na Bwana Kenyatta – walikuwa na uhasama mkubwa wa kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017 – walikubaliana kufanya kazi pamoja mwaka 2018 kwa ajili ya “kuteta amani nchini “.

Uhusiano wa karibu wa Bwana Kenyatta na Bwana Odinga na pia kuongezeka wa umaarufu wa Bwana Odinga tangu walipofanya makubaliano kunaangaliwa na baadhi ya watu kama njama za kisiasa za kumaliza mpango wa Bwana Ruto wa kumrithi Bwana Kenyatta kama rais.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents