Tia Kitu. Pata Vituuz!

Akon athibitisha kufikia makubaliano ya kuanza kujenga mji wake nchini Senegal ‘ Akon City’

Akon athibitisha kufikia makubaliano ya kuanza kujenga mji wake nchini Senegal ' Akon City'

Mwanamuziki maarufu kutoka Marekani Aliaune Damala Bouga Time Puru Nacka Lu Lu Lu Badara Akon Thiam, Alimaarufu Akon, amethibitisha kwa kuameandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa mipango yake ya kujenga mji wake nchini Senegal, nchi asili ya familia yake, inaendelea na amefikia katika hatua za mwisho za makubaliano ya ujenzi wa mji huo ambao unatarajiwa kupewa jina la ‘ AKON CITY ‘

Akon ameeleza kuwa amekamilisha makubaliano ya mji wake kujengwa katika nchi hiyo iliyopo Magharibi mwa bara la Afrika.

 

Licha ya kuthibitisha ujenzi wa mji huo bado hakuna maelezo mengi kuhusu mipango ya mji huo, ambao umekuwa ukiongelewa tangu mwaka 2018 alipozindua sarafu zake za kidijitali zinazoitwa ‘’Akoin’’.

Kwa wakati huo Akon alisema anataka kujenga mji wenye muonekano kama mji wa “Wakanda halisi” ambao ulionekana katika movie ya ‘Black Panther’ muonekano wa mji huo ukionekana pia  nyuma ya sarafu hiyo, ikiwa kama kumbukumbu ya nchi ya Wakanda, ambayo ilitengenezwa na kampuni ya filamu ya Marvel, ndani ya filamu ya Black Panther.


Aliwaambia mashabiki wake kuwa amezawadiwa ekari 2,000 za eneo na mamlaka nchini Senegal, ili kuanza kujenga mradi huo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW