Tupo Nawe

Al-shabaab waua na kuteka Madaktari wawili nchini Kenya

Askari mmoja ameuawa papo hapo kwa kupigwa risasi na wanaume waliokuwa wamebeba silaha za moto wanaosadikika kuwa ni wanamgambo wa Alshabaab huko mjini Mandera nchini Kenya.

Wanaoshukiwa kutekwa ni Dr Assel Herera Correa (General Physician) kulia na Dr Landy Rodriguez (Surgeon) kushoto

Taarifa za awali zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Kenya zinaeleza kuwa kwenye tukio hilo, madaktari wawili raia wa Cuba wametekwa kwenye tukio hilo.

Tukio hilo limetokea mapema leo Aprili 12, 2019 asubuhi wakati madaktari hao wakielekea kazini katika mji huo uliopo katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya.

Washambuliaji hao walikuwa na gari aina ya Probox ambalo kwa mujibu wa mashuhuda gari hilo, lilikuwa limeegeshwa nje ya makazi hayo ya madaktari.

Milio ya risasi imesikika katika mji wenyewe wa Mandera na kwa sasa maafisa wa usalama wanawasaka watekaji hao.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW