Habari

Alaine kutoka Jamaica aliyeshirikishwa na Wyre katika ‘Nakupenda Pia’, ndiye msanii wa pili wa Kimataifa atakayekuwepo Serengeti Fiesta 2013 Dar

Baada ya Davido wa Nigeria kutangazwa jana kuwa atakuwepo katika fainali za Serengeti Fiesta jijini Dar es salaam, msanii mwingine wa kimataifa kutoka Jamaica Alaine ameongezeka katika orodha ya wasanii wa kimataifa watakaokuwepo kutumbuiza.

alaine2
Alaine

Alaine ni msanii wa kike aliyeshirikishwa katika wimbo uliojipatia umaarufu mwaka huu ‘Nakupenda pia’ kutoka kwa love child Wyre wa nchini Kenya. Kwa msaada wa single hiyo miezi michache iliyopita Alaine aliperform Katika majukwaa ya Kenya pamoja na Uganda na sasa ni zamu ya Tanzania.

Serengeti Fiesta italitikisa jiji la Dar es salaam Jumamosi ya wiki ijayo October 26 katika viwanja vya Leaders.

Alaine

Mfahamu Alaine
Alaine ambaye jina lake kamili ni Alaine Laughton ni mwimbaji wa reggae aliyezaliwa New Jersey, Marekani na baadae kuhamia Jamaica akiwa na miaka mitatu.

Miaka ya 1990 na mwanzoni mwa 2000 Alaine aliishi tena Marekani, na akiwa huko alishiriki katika uandishi wa nyimbo pamoja na kuwafanyia backup wasanii wa Rocafella wakiwemo Cam’ron pamoja na Freeway.

Alaine mwenye miaka 35 pia amewahi kushiriki katika movie ya mwaka 1988 ‘Clara’s Heart’ ambayo starring alikuwa Whoopi Goldberg.

Mwaka 2004 Alaine alirejea Jamaica na kuanza kufocus katika muziki wake.

Jina lake limekuwa zaidi Afrika Mashariki baada ya kushirikishwa na Wyre katika single iliyohit nchi zote tatu za Kenya, Uganda na Tanzania yenye maneno ya Kiswahili ambayo Alaine aliyaimba ‘Nakupenda pia’.

Moja ya single zake za reggae zilizofanya vizuri ni pamoja na ‘You are me’ aliyoitoa kama dedication kwa mama yake

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents