Michezo

Alan Pardew kocha mpya West Bromwich

Uongozi wa klabu ya West Bromwich Albion wathibitisha Alan Pardew kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

Pardew ambae alikuwa kocha wa West Han United, Charlton, Athletic, Newcastle United na Crystal Palace anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tony Pulis aliyefukuzwa kazi baada ya kushinda mechi mbili kati ya michezo 21 toka awemeneja wa timu hiyo.

Pardew amesema “Ninafuraha kuona nimepata nafasi ya kukifundisha kikosi cha Albion kilichojaa wachezaji wengi wenye vipaji.”

“Changamoto yetu ya kwanza ni kuhakikisha tunapata matokeo yatakayo tuwezesha kupanda katika msimamo wa ligi lakini pia nafahamu kujiunga kwangu hapa ni muhimu kwa kuhakikisha ninasogeza mbele gurudumu hili.”

Mchezo wake wa kwanza, Pardew atakabiliana na timu yake ya zamani ya Crystal palace  siku ya Jumamosi huku akiwa na wasaidizi wake John Carver katika benchi la ufundi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents