Picha

Albam ya Justin Timberlake yauza kopi 968,000 katika wiki ya kwanza

Albam mpya ya Justin Timberlake, “The 20/20 Experience” imekamata nafasi ya kwanza kwenye Billboard 200 chart, kwa kuuza kopi 968,000 katika wiki yake ya kwanza, kwa mujibu wa Nielsen SoundScan.

justin-timberlake-the-2020-experience-photo-shoot-tom-munro-main-600x450

“20/20,” ilitoka March 19, na ndio albam aliyouza zaidi katika wiki ya kwanza. Albam yake ya mwaka 2006 “FutureSex/LoveSounds,” iliuza kopi 684,000 na ile ya kwanza aliyoitoa mwaka 2002, “Justified,” iliuza kopi 439,000.

Mauzo huzo hayo ya “20/20’s” ni makubwa zaidi tangu SoundScan ianze kuchukua data za mauzo ya albam mwaka 1991.

Albam ya kundi la zamani la Timberlake, ‘N Sync, “No Strings Attached” iliuza kopi milioni 2.42 katika wiki ya kwanza na kukamata na kuongoza chart ya Billboard 200, April 8, 2000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents