Burudani

Albam ya Rihanna ‘Unapologetic’ yakamata nafasi ya kwanza kwenye chart za Billboard

Rihanna amefanikiwa kuiingiza moja kwa moja albam yake mpya Unapologetic kwenye chart za albam 200 za Billboard.

“Unapologetic,” iliyokamata nafasi ya kwanza pia kwenye iTunes katika nchi 43 ikiwa masaa tu tangu itoke November19, iliuza kopi 238,000 kwa mujibu wa Billboard.

Wimbo wa kwanza kutoka kwenye albam hiyo, “Diamonds” upo kwenye top five ya Billboard Hot 100 wiki iliyopita na kuwa single ya 12 ya Rihanna kuwahi kukamata nafasi ya kwanza.

Albam hiyo imefanyiwa promotion ya uhakika na Rihanna aliyefanya ziara ya siku saba kwenye majiji saba duniani kote kwa kusafiri na waandishi wa habari pamoja na mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents