Albino Chupuchupu Kutekwa

Mlemavu wa ngozi, Dunia Kubingwa (36), mkazi wa kijiji cha Katoro wilayani hapa Mkoa wa Mwanza amenusurika kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kumnywesha pombe na kulewa chakari hadi kupoteza fahamu.

Mlemavu wa ngozi, Dunia Kubingwa (36), mkazi wa kijiji cha Katoro wilayani hapa Mkoa wa Mwanza amenusurika kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kumnywesha pombe na kulewa chakari hadi kupoteza fahamu.

Kubingwa ambaye kwa sasa analala katika Kituo cha Polisi cha Katoro kwa usalama wake, alinusurika kuuawa baada ya kuokolewa mikononi mwa watu wanaodaiwa kumbeba mzobemzobe usiku baada ya kumnywesha pombe.

Akizungumza na PST jana asubuhi kwenye Kituo cha Polisi cha Katoro, Kubingwa amedai mkasa huo umemfika usiku wa kuamkia jana wakati anatoka kituo cha polisi cha Katoro kutoa taarifa ya kuangukiwa na kifusi cha choo na kujeruhiwa mwili.

Alidai kuwa baada ya kutoa taarifa hiyo polisi wakati akiwa njiani kurejea nyumbani majira ya jioni mtu mmoja anayemtambua kwa jina la Kibisha Ng`wandi (36), mkazi wa kijiji cha Katoro, alimwita apite kwenye baa alipokuwa akinywa pombe na wenzake, iitwayo Saanane.

Aliongeza kuwa baada ya kufika hapo walianza kumnunulia bia kabla ya kuhamia kwenye pombe ya kienyeji maarufu kwa jina la Kangara nyumbani kwa mama mmoja ambako alikunywa hadi kulewa chakari.

Kubingwa alidai anachokumbuka ni kuwa ilipofika majira kati ya saa tatu na saa nne usiku, watu wanne akiwamo mwenyeji wake aliyemtaja walimtaka kuondoka naye kusikojulikana kwa vile alikuwa hajiwezi hakuwa na chaguo, ndipo walipoondoka naye.

Pia alidai kuwa kutokana na kulewa kupita kiasi watu hao walimshika na kumpeleka mzobemzobe wakiwa wamshikilia kwani alikuwa amelewa kiasi cha kujikojolea.

Hata hivyo, kutokana na kuwepo kwa hali hiyo inadaiwa raia mwema alitoa taarifa kituo cha polisi cha Katoro na hivyo Polisi kumwokoa kutoka mikononi mwa watu hao.

Baada ya polisi kufika eneo la tukio inadaiwa wengine walitoweka, lakini mwenyeji wake ambaye ndiye aliyemwita alitiwa mbaroni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo kwa njia ya simu alidai alikuwa hajapokea taarifa rasmi kuwepo kwa tukio hilo na kuahidi atafuatilia na kulitolea ufafanuzi.

Habari kutoka ndani ya polisi wilayani hapa zimethibitisha kushikiiliwa kwa Kibisha Ng`wandi kuhusiana na tukio hilo kwa lengo la kumhoji.

Tayari waganga wa jadi watatu waliotambuliwa kwa majina ya Mayala Lubuna (69) na Jangu Kamoja (74) wote wakazi wa kijiji cha Nyaruyeye na Mhangwa Ndekanilo (26) mkazi wa kijiji cha Lwamgasa wamekamatwa wiki iliyopita kwa tuhuma za kuendesha vitendo vya upigaji ramli vinavyodaiwa vinaweza kuchochea mauaji ya vikongwe na albino.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents