Burudani

Album mpya ya Kanye West “Yeezus” yakamata nafasi ya kwanza katika chati za Billboard 200 katika wiki yake ya kwanza

Wiki iliyopita (June 18) rapper Kanye Kanye West alifanikiwa kuingiza sokoni album yake mpya ya 6 “Yeezus” ambayo mpaka jana (June 25) ikiwa imefikisha wiki moja imeweza kuuza nakala 327,000 na kukamata nafasi ya kwanza katika chati za Billboard 200.

Kanye West

Kwa mujibu wa Nielsen SoundScan, “Yeezus” ndio album ya rap iliyoweza kushika nafasi ya kwanza toka album ya Drake “Take Care” kukamata nafasi hiyo mwezi November (2011) kwa mauzo ya kopi 631,000 .

Lakini pamoja na “Yezuus” kushika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard 200, kwa upande wa Kanye ndio album yake ya 1 kuwa na mauzo madogo kupita zote katika wiki ya kwanza ya mauzo, ambayo inazidiwa na album yake ya “The College Dropout” ya mwaka (2004) iliyouza nakala 441,000 katika wiki yake ya kwanza na kushika nafasi ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents