Burudani
Album ya Kanye West ‘The Life of Pablo’ yaweka historia
Album ya Kanye West, The Life of Pablo imeweka historia. Imekuwa album ya kwanza iliyotoka mtandaoni pekee kwenda platinum, kwa uthibitisho wa Recording Industry Association of America, RIAA.
Kwa mujibu wa label yake, Def Jam, Kanye amepata cheti cha platinum baada ya album hiyo kusikilizwa mtandaoni mara bilioni 3, kutosha kuifanya ifikie sawa na units milioni moja za mauzo ya kawaida.