Burudani

ALERT: Kolabo kubwa mbili zinakuja, Diamond ft Harmonize na Ommy Dimpoz ft Alikiba

Kama wewe ni shabiki au mdau wa muziki wa Bongo Fleva, basi mwaka huu utauanza vizuri kwani kuna kolabo kubwa mbili zinakuja za wasanii wakubwa hapa Tanzania.

Kolabo ya kwanza ni ya Ommy Dimpoz na Alikiba, tayari wawili hao wameshaingia locations nchini Oman ku-shoot video ya kolabo hiyo.

Hii ni kolabo ya tatu ya wawili hao, ambayo watu wengi wanaisubiri kwa hamu baada ya kolabo zao mbili za wimbo wa Nai Nai na Kajiandae kufanya vizuri.

Kolabo nyingine kubwa inayosubiriwa kwa hamu ni ya Diamond Platnumz na Harmonize.

Hii inakuwa ni kolabo ya tatu kwa wasanii hao kutoka WCB, hii ni baada ya kufanya vizuri na kolabo mbili za Bado na Kwangwaru.

Imeelezwa kuwa Diamond na Harmonize wiki hii wameanza ku-shoot video ya kolabo hiyo Jijini Dar Es Salaam.

Je, unadhani kolabo ya Diamond Ft. Harmonize itavunja rekodi ya Kwangwaru? au kolabo ya Ommy Dimpoz Ft. Alikiba itakuwa kali kuliko ile ya Kajiandae.?

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents