Michezo

Alex Iwobi na Wizkid wazitambulisha jezi za timu ya taifa zilizo tengenezwa na kampuni ya Nike (+picha)

Timu ya taifa ya mchezo wa mpira ya nchini Nigeria iitwayo Super Eagles wazindua jezi zitakazo tumika katika Kombe la Dunia 2018 . Jezi hizo zimezinduliwa rasmi na kampuni ya Nike pamoja na Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF).

Nike kwa sasa ndiyo kampuni rasmi inayodhamini timu hiyo ya taifa la Nigeria.

Mtengenezaji wa jezi hizo aliziwasilisha jezi hizo kwa NFF kwenye sherehe iliyo fanyika huko jijini London siku ya jana Jumatano.

Jezi Super Eagles zitakazo tumika kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu zilivaliwa kwa mara ya kwanza na mshambuliaji wa timu ya Arsenal Alex Iwobi pamoja na mwanadada Sophia Omidiji aliyevaa jezi za timu ya wanawake la taifa hilo Super Falcons.

Timu ya Super Eagles itakutana uso kwa uso na timu ya Argentina, Croatia na Iceland katika kikundi D kwenye Kombe la Dunia litakalo fanyika juni mwaka huu.

 


Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents