Soka saa 24!

Alex Sanchez akata ukimya awaangukia mashabiki wa Man United,asingizia majeraha, awatupia lawama wanahabari kuandika uongo kuhusu yeye

Alex Sanchez akata ukimya awaangukia mashabiki wa Man United,asingizia majeraha, awatupia lawama wanahabari kuandika uongo kuhusu yeye

Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Chile Alexis Sanchez, 30, aliyesajiliwa kutoka Arsenal ya hapo hapo Uingereza huku akipokea kitita cha £400,000 kwa wiki ameonyesha kiwango kibovu sana msimu huu katika klabu hiyo kitu ambacho watu hawakutegemea kutokana na kiwango cha nyota huyo.

Ikiwa ndio msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo matokeo yake wameipeleka timu katika nafasi ya 6 ya ligi hiyo, Sanchez alilaumiwa sana kwa kuonyesha kiwango hafifu ingawa majeruhi pia yalimuandama lakini haikiwa sababu ya kuonyesha kiwango duni katika klabu hiyo.

Ikiwa msimu umemalizika mchezaji huyo amechukua fursa ya kuwaomba mashabiki wa timu hiyo msamaha kwa kutoonyesha kiwango chake chote, alex ameandika hivi:-

“Kiukweli ulikuwa msimu mgumu sana …”Mashabiki ndio ambao wanastahili kuombwa msamaha kwa sababu wao wanakuunga mkono bila kujali nini kinachotokea. Bila shaka, sikufanya kama vile nilivyotarajia kwa sababu ya majeraha yasiyotabirika.

“Lakini kitu ki gine Waandishi wa habari na watu walikuwa wakizingatia mambo yasiyokuwa ya kweli. Nilikuwa mtaalamu katika vipengele vyote nawaombea mashabiki kwa kuwa hawawezi kufikia malengo yetu.

“Wachezaji na wafanyakazi wanauliza kama tulikuwa tukifanya jambo linalofaa na kama tungeweza kufanya kitu na kutoa kila kitu tulichonacho ili kufanya kitu bora zaidi tukiwa tumevaa jezi hii ya klabu hii bora kabisa ya soka duniani… Nina hakika kwamba Manchester United siku moja itarudi kuwa klabu, kama ilivyokuwa siku za zamani ikiwa na kocha bora Sir Alex Ferguson. ”

Hayo ndio yalikuwa maneno ya Sanchez kwa Mashabikiwa Manchester United.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW