Michezo

Alexandre Pato: Nafurahia sana kuwa Chelsea ndio makao yangu mapya

Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imekamilisha usajili wa mkopo wa mshambuliaji wa Corithians Alexandre Pato.

Mshambuliaji huyo wa Brazil amehamia Stamford Bridge mpaka mwisho wa msimu huu huku kukiwa na nafasi ya kumsajili moja kwa moja kwa ada ya pauni milioni sana majira ya joto.

pato4

Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan, 26, aliwasili Uingereza wiki hii usiku kwa majaribio kabla ya kutia sahihi mkataba wa muda hadi mei.

“Natamani sana kuichezea Chelsea. Nahitaji kucheza. nafurahia sana uhamisho huu.” alisema Pato.

Pato alijiunga na AC Milan mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 17.

Hata hivyo alishindwa kufanya vizuri kama ilivyotarajiwa na ikambidi kurejea Brazil mwaka wa 2013.

Tayari amefunga mabao 10 katika mechi 25 alizoichezea Brazil,

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents