Michezo

Alexis Sanchez ajipanga kivingine, apiga mazoezi makali na mbwa (+Picha)

Wakati wapenzi wa soka duniani wakielekeza macho na masikio yao kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi, nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez anazidi kujiimarisha kwaajili ya msimu ujao baada ya kuonekana akifanya mazoezi makali na mbwa wake nchini Chile.

Sanchez ambaye hayupo kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya timu yake ya taifa ya Chile kushindwa kufuzu, winga huyo ameonekana nyumbani kwao akifanya mazoezi makali.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 29, kwa sasa yupo na mbwa wake Atom na Humber. Baada ya kupitia kwenye kipindi kigumu mwanzo wa safari yake ya maisha ndani United, Sanchez atalazimika kufanya mazoezi makali ili kuweza kuwa muhimu kwa meneja, Jose Mourinho msimu ujao.

Sanchez amejiunga na United akitokea Arsenal mwezi Januari baada ya kubadilishana na Henrikh Mkhitaryan. hata hivyo Sanchez ametumia jitihada kubwa sana mpaka kuwa sawa na kufanikiwa kufunga mabao matatu na pasi tano zilizochangia mabao katika michezo 18 aliyoitumikia United msimu uliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents