Michezo

Alexis Sanchez aweka rekodi ya kufunga Hat-trick katika ligi tatu tofauti

Mshambuliaji Alexis Sanchez wa Arsenal ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick katika ligi kuu tatu tofauti duniani, Serie A, La Liga na EPL.

Alexis Sanchez

Hat-trick yake ya kwanza ilikuwa wakati anaichezea Udenise ya Italia ambapo waliifunga Palermo mabao 7-0 katika mchezo wa ligi kuu soka nchini Italia mwaka 2011. Hat-trick ya pili ameipata akiwa na Barcelona nchini Hispania ambapo waliifunga Elche mabao 4-0.

Magoli matatu ya Sanchez ya weekend hii ni baada ya kuisadia timu yake Arsenal na kuifunga Leicester 5-2 iliyokuwa haijafungwa hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents