Michezo

Alexis Sanchez kuibeba Arsenal mabegani mwake

By  | 

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez, ameisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa magoli 2 kwa 0 dhidi ya Sunderland, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Emirates na hivyo kuiwezesha klabu hiyo kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya.


Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza.

Sasa Gunners inahitaji kuwashinda watoto wa, David Moyes, ili waweze kufanikiwa kumaliza katika nafasi nne za juu za ligi kuu nchini Uingereza.

Katika mchezo huo ulioonekana kuwa mgumu, Sanchez aliwezesha klabu yake kuchomoza na ushindi huo. Arsenal iliyopo katika moto mkali chini ya kocha wake, Arsene Wenger, hakuwahi kumaliza nje ya nne bora katika misimu yote.


Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez akishangilia baada ya kufunga goli la pili

Kwa ushindi wa Manchester City’s dhidi ya West Brom unatoa tafsiri ya klabu ya Arsenal kuhitaji ushindi wa lazima katika mchezo wao wa jumapili dhidid ya Everton huku akiombea mabaya Liverpool katika mchezo wao dhidi ya Middlesbrough.

Bado kuna siri kama Mzee Wenger ataendelea kusalia katika nafasi hiyo ya kocha, fumbo hili litafumbuliwa mpaka itakapo tangazwa kama atasaini Mkataba mpya ndani ya Arsenal, mpaka sasa mashabiki wa klabu hiyo hawataki kuona Mzee huyo akiendelea kusalia ndani ya klabu ya The Gurners.

BY HAMZA FUMO

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments