Burudani

Ali Kiba hataki show Bongo

Ali Kiba ameweka wazi kwamba kwa sasa hana time na show za kibongo kwa sababu baadhi ya mapromota wameonesha tabia za wizi na kudhulumu haki za wasanii, “Unajuwa muziki bongo unalipa tu kwa kuuza kazi zako, lakini haya mambo ya show kumekuwa na ubabaishaji mwingi ndiyo maana unaona nakuwa mgumu sana kufanya show za hapa nchini” alisema Kiba.

Mkali huyu wa Bongo Flava kwa sasa anaongoza kwa kupiga show za Ughaibuni, licha ya kutopiga show bongo kazi zake bado zinauzika hapa na nchi za jirani bila shida.

“Kuna watu fulani fulani hivi wanawaumiza sana wasanii, huku wakitangaza kuwasaidia na kuwainua, lakini ukweli ni kuwa jamaa ni watu wa dhuluma sana ndiyo maana mimi nakamua mbele kwa mbele ambako hakuna longolongo,” alieleza Kiba.

Ali Kiba aliendelea kusema kwamba kwa sasa haonekani mitaani kwa sababu anaanda nyimbo za album mpya na wapenzi wake wakae mkao wa kula!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents