Michezo

‘Ali Kiba ni mtu wa kazi tu’ – Simon Msuva

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Simon Msuva amefunguka na kusema kuwa yeye ukitaja msanii wa muziki hapa Bongo basi hawezi kusita kumtaja Ali Kiba kwani ni Msanii ambae anawakilisha nchi kimataifa.

Image result for simon msuva
Simon Msuva (Jezi ya Kijani) akiwatoka Mabeki wa Azam FC kwenye moja ya Mchezo wa Ligi Kuu msimu huu.

Msuva amesema kuwa kwa hapa Bongo kuna Wasanii wengi wanaofanya vizuri lakini mahaba yake ni kwa Ali Kiba kwani ana sauti nzuri, anajituma kwenye kazi zake na sio mtu wa maneno maneno.

Namkubali sana Ali Kiba anafanya muziki wake kimataifa zaidi yaani kuanzia utunzi wake,anavyojituma kwenye kazi zake pia sio mtu wa maneno maneno yeye ni mtu wa kazi tu“,Alisema Simon Msuva kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.

Simon Msuva anayekipiga kunako Klabu ya Yanga msimu huu ameibuka na tuzo ya mfungaji bora akiwa na magoli 14.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents