Burudani

Alice ni mshindi wa Miss Dar Indian Ocean


Aliyekuwa mmoja kati ya warembo washiriki katika kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Dar Indian Ocean Alice Lushiku ameibuka kidedea baada ya kuwapiga chini warembo wenzake kumi na tatu (13) waliokuwa nae kwenye kinyng’nyiro hicho.

Mashindano hayo ya kumsaka mlimbwende wa Dar Indian Ocean yalianza kupamba moto mida ya saa nne usiku jana tarehe 10/06/2010 pale warembo wote kumi na nne (14) walipo pita mbele ya majaji na mashabiki waliohudhuria katika shoo hiyo iliyyofanyika kwenye hoteli ya Double Tree Hilton pale masaki jijini Dar es salaam.

Mashindano yalikuwa ni ya aina yake kutokana na kile kilichozoeleka kwamba mashindano ya urembo ni lazima kuwe na jukwaa kwa ajili ya warembo kupita lakini kwa pale ilikuwa ni tofauti kwani warembo walianza kutokea juu ya ngazi na kuteremka chini kisha kupita mbele ya mashabiki ambao walikuwa wamekaa huku na huku na kuacha nafasi katikati ambayo ndiyo iltumika kwa warembo hao konyesha manjonjo yao.

Mpambano ulikuwa mgumu sana kwani kila mmoja wa warembo alikuwa amejiandaa vya kutosha ila mwisho wa yote ilikuwa ni lazima mshindi apatikane.…….Umeona eeeeeh!?

Basi warembo walikuja kujitambulisha mmoja mmoja na baadae kupita na aina tofauti tofauti ya mavazi kisha kwenda kusubiri majaji wafanye kazi yao. mavazi waliyopita nayo warembo ni pamoja na vazi la jioni, vazi la ufukweni na vazi maalum lililoabuniwa na na Bi. Asia Hidarus ambaye ndie alisimamia mpango mzima wa kuwapendezesha warembo. Pia palikuwa na buurudani kutoka T.H.T ambao walileta burudani ya kutosha kabisa ikiwa ni kuanzia kudansi mpaka uimbaji. Waimbaji waliokuwepo ni Linah na R. Tone wote kutoka T.H.T.

Baada ya hapo mchujo wa kwanza ulipita na kubakisha warembo tisa (9) ambao walichuana na kasha kubaki watano (5) ambao pia walichuana kwa mfumo wa kuulizwa maswali na baadae mshindi kutangazwa ambaye  ni Alice Lushiku.

Kuacha Alice lushiku ambaye ndio mshindi wa kwanza pia kuna Irene Ezron ambae alikuwa mshindi wa pili huku akichukua taji la face of Robialac, pia kuna Edna Kwilasa yeye alikuwa mshindi wa tatu na Nuria ahmed alishika nafasi ya nne huku nafasi ya tanio ikichukuliwa na mwanadada Happywhitney Hendru.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents