Alichojibu Amber Rose kuhusu kuachana na mpenzi wake

Video vixen na mwanamitindo wa Marekani, Amber Rose amejibu tuhuma  zinazozagaa za kuachana na mpenzi wake.

Amber amekanusa tuhuma hizo za kutemana na rapper 21 Savage zilizotolewa na mtandao wa ‘The Shade Room’ hivi karibuni, na kusema yeye na rapper huyo bado wana mahusiano.

“I just unfollowed over 100 people though. His unfollow was on accident—It’s back up now”, amesema Amber.

Licha ya kuwa bado hakuna uhakika wa wawili hao kuwa wapenzi ila ripoti inaonyesha kuwa wawili sio marafiki tena katika mtandao wa kijamii wa Instagram na wamefuta picha za kila mmoja wao.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW