Alichokiandika Wizkid kuhusu kifo cha Radio

Wizkid ameonyesha kugusa sana na kifo cha msanii wa Uganda ambaye amedumu kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 10, Moses Ssekibogo maarufu kama Mowzey Radio ambaye amefariki jana (Alhamisi).

Wizkid ameonyesha hisia zake za kuumizwa na msiba huo, kutokana na ujumbe ambao ameuandika kupitia mtandao wake wa Instagram ukiwa unaosomeka, “Rest in paradise my brother Radio! 💔…Speechless… Love u forever star! ❤️ !! Nothing can ever be the same! 💔! Superstar lives forever…🖤🖤🖤.”

Radio alilazwa katika Hospital Kuu ya Uganda akipatiwa matibabu tangu January 23 mwaka huu ambapo hali yake ilidaiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi uliotokea klabu huko mjini Entebbe.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW