Burudani

Alichosema Bill Nass kuhusu Akwelina (+video)

Hapo jana katika viwanja vya Chuo cha NIT uliangwa mwili wa mwanafunzi Akwelina Akwilini ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano.

Kifo cha mwanafunzi huyo ambaye amezikwa leo katika kijiji cha Kitowo kata ya Marangu, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, kiliwaguswa watu wa aina tofauti tofauti miongoni mwao ni wasanii.

Hapo jana katika kuuaga mwili wa Akwelina alionekana msanii msanii Bill Nass. Rapper huyo amefunguka haya.

“Niliguswa sana sana na kwa mapenzi yangu kama kijana hao ni watu wanapenda miziki yetu, mtu kama yeye alikuwa chuo alikuwa na ndoto na alikuwa akitafuta namna ya kutimiza kwa hiyo kwangu mimi niliguswa”,  Bill Nass ameiambia Bongo5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents