Burudani

Alichosema Dkt. Tulia Ackson kuhusu Mange

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema hana uhakika iwapo dada maarufu mtandaoni Mange Kimambi ni binadamu wa kawaida.

Akizungumza katika kipindi cha Maisha Mseto kinachorushwa Times Fm amesema kutokana na hilo hawezi kusema iwapo anakosea kwa kile anachokifanya.

“Sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye ndiyo nitajua chakuzungumza naye lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata fursa ya kumshauri nikionana naye,” amesema.

“Siwezi kusema anakosea kama nilivyosema sijajua yeye ni mtu wa namna gani kwa hiyo huenda hakosei labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti hivyo kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents