Burudani ya Michezo Live

Alicia Keys awa mkurugenzi wa ubunifu wa Blackberry + Jay-Z amsainisha Timbaland Roc Nation

alicia

Pamoja na kuachia hit baada ya hit na kuperform katika kila tukio kubwa nchini Marekani, Alicia Keys jana ametajwa kuwa mkurugenzi wa ubinifu wa simu za Blackberry duniani.

Keys alipewa cheo hicho kwenye uzinduzi wa Blackberry 10 huko New York na mwenyekiti mtendaji wa RIM, Thorsten Heins.
Katika cheo chake, Alicia atakuwa akifanya kazi kwa ukaribu na watengenezaji wa applications za simu hizo, waundaji wa content, wauzaji, pamoja na jamii ya burudani ili kuboresha umaarufu BlackBerry.

alicia 3

Baada ya kupewa shavu hili Alicia alitweet: Excited2jump right in2my new role as Global Creative Director [email protected]! #BlackBerry10 #keepmoving #forwardthinking

Katika hatua nyingine kubwa jana baada ya Timbaland kuwa mpishi wa midundo ya Jay-Z kwa karibu miaka 15 mpaka sasa, hatimaye Jay ameamua kumchukua kwenye familia yake ya Roc Nation.

jay-timbo_zps29e1f7ce

Rapper huyo alitumia website yake Life+Times jana kutangaza habari hizo pamoja na picha hiyo juu kwa kuandika: “Roc Nation welcomes TIMBALAND to the family.”

Timbo pia alitengeneza wimbo mpya wa Justin Timberlake Suit & Tie ambao Jay-Z ameshirikishwa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW