Habari

Alicia Keys kutumbuiza nchini Israel mwezi July, licha ya kupewa vitisho na kushauriwa kuahirisha

Muimbaji wa R&B Alicia Keys amesema ataendelea na ratiba yake ya kutumbuiza nchini Israel mwezi ujao kama alivyopanga, licha ya kupokea maoni ya watu kadhaa wakiwemo wanamuziki wakimtaka aahirishe kutumbuiza nchini humo.

Alicia

Hit maker huyo wa ‘girl on fire’ anategemea kutumbuiza Tel Aviv, July 4 ikiwa ndio ziara yake ya kwanza nchini Israel, lakini amepokea vipingamizi kutoka kwa mwanamuziki Roger Waters na mwandishi wa ‘The color purple’ Alice Walker ambao wamemuomba kupitia barua ya wazi ‘open letter’ asiendelee na mpango wake wa kutumbuiza Israel.

Katika barua hiyo yenye maneno 400 iliyowekwa katika mtandao wa kikundi kinachoitwa ‘the Palestinian Campaign for the Academic & Cultural Boycott of Israel’ Mr. Waters amemuomba ms Keys asiipe serikali ya Israel nafasi ya kulitumia jina lake kupromote sera za kibaguzi dhidi ya Palestina.

Waters, ambaye hivi karibuni alikuwa miongoni mwa watu waliomshawishi Steve Wonder kutotumbuiza katika tamasha la kukusanya fedha kwaajili ya marafiki wa majeshi ya ulinzi ya Israel, alisema “tunatakiwa kusimama kwa pamoja na kaka zetu na dada zetu dhidi ya ubaguzi wa rangi, na ukoloni”

Walker, ambaye ni wakili wa the Palestinian Campaign for the Academic & Cultural Boycott of Israel, amemuonya Keys kuwa anachotaka kufanya ni kuweka roho yake hatarini kwa kwenda kutumbuiza katika nchi aliyoiita ya ubaguzi wa rangi “an apartheid country.”

Ushauri huo haujamwingia Alicia Keys ambaye amesema yeye anaamini kuwa muziki unaweza kusaidia kuleta amani.
“I look forward to my first visit to Israel. Music is a universal language that is meant to unify audiences in peace and love, and that is the spirit of our show,” Alicia Keys aliuambia mtandao wa New York Times.

Wanamuziki wengine ambao wamewahi kupokea vipingamizi vya kufanya maonesho nchini Israel ni pamoja na Elton John na Rihanna, ambao hata hivyo walitupilia mbali maoni hayo na kuendelea na show zao nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents