Tupo Nawe

Alikiba afunguka kuhusu ugomvi wake na mke wake ‘Ni kweli kuna ungomvi ila sijaachana nae, mi napenda wanawake’ – Video

Alikiba afunguka kuhusu ugomvi wake na mke wake 'Ni kweli kuna ungomvi ila sijaachana nae, mi napenda wanawake' - Video

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ali Salehe Kiba alimaarufu Ali Kiba amefunguka mwanzo mwisho kuhusu kinachoendelea katika familia yake na hasa kuhusu kile kilichosemekana kuwa ameachana na mke wake.

Akiongea katika kipindi cha Ala za roho kinachoruka Clouds Fm Alikiba ameongea mengi sana na kusema:- “Sijaachana na mke wangu kama ambavyo watu wanadai bali nimemruhusu aende kwao nchini Kenya kufanya kazi” mbali na kuzungumzia hilo pia amefunguka jinsi anavyojisikia watu wanavyomsema mama yake na kuhusishwa katika ugomvi wake na mke wake na sio kwamba mama yake ndio chanzo cha kila kitu kuhusu kuachana na mke wake “Mama yangu hausiki kabisa katika ugomvi huu na mama ndio mtu pekee ambaye alikuwa anatusuluhisha kwamba jamani malizeni haya mambo, lakini anaposikia watu wanavyomzungumzia hivi mi najisikia vibaya sana na hata mama yangu hayuko sawa mpaka sasa hivi kutokana na haya maneno, tuwaheshimu wazazi wetu jamani ukiona mtu anaongea hivi ujue hajafunzwa vizuri na wazazi wake”

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW