Burudani

Alikiba akubali mwaliko wa Diamond kwenye Tamasha la Wasafi Festival kwa hiki alichokiandika ?

Alikiba akubali mwaliko wa Diamond kwenye Tamasha la Wasafi Festival kwa hiki alichokiandika ?

Baada ya C.E.O wa Wasafi Diamond Platnumz kutangaza kuwa anatamani sana kumuona msanii mwenzake pia akiwa kama kaka yake kwenye muziki Alikiba awepo kwenye tamasha lake la Wasafi Festival ambalo linatarajiwa kuanzishwa mwezi wa 11 tarehe 24 mwaka huu ambalo linatarajiwa kuanzia mkoani Mtwara.

Diamond alisema ” Hili tamasha ni lakwetu sote kwa wasanii wote wa Kitanzania na katika tamasha hili ningefurahi sana kama kaka yangu Alikiba atakuwepo kwenye Tamasha hili”

Lakini baada ya Diamond kuongea hayo watu walianza kuzungumza mitandaoni na kuanza kusema Alikiba hawezi kukubali huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana.

Usiku wa kuamkia leo Alikiba alipost kwenye ukurasa wake wa Instagram picha ya mchekeshaji maarufu sana kutoka kutoka Marekani Mr Benn,ambayo inasomeka ” Thank you for listerning to my presentation”

halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”

Je kwa post hii na hichi alichokiandika inamaanisha kuwa Alikiba amekubaliana na ombi hili la Diamond ?

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents