Burudani

Alikiba amesema kuwa muziki wa Bongo Flava umepungua kasi ‘Kuna watu wanaharibu muziki’

Msanii wa muziki nchini, Alikiba amesema kuwa mwendo wa muziki wa Bongo Flava umepungua kasi siku za hivi karibuni kutokana na kukosekana kwa tuzo ambazo zilikuwa zikichangia sana kuhamasisha Watanzania.

Alikiba anayetamba na kibao chake cha Mvumo wa Radi ameyasema hayo katika mahojiano na Azam Tv mwezi huu wa Agosti kupitia kipindi cha Nyundo ya Baruan.

”Mwendo wa muziki wa Bongo Flava unakwenda vizuri ijapokuwa kuna watu wanachanganya tu muziki na wengine wanaaribu muziki na wengine wanakwenda nao vizuri lakini hiyo pia siwezi kuichambua kwa sababu kila mtu anakipaji chake,” amesema Alikiba

Alikiba ameongeza ”Wengine wanafanya kwa kujifurahisha na wengine wanafanya kwaajili ya maisha yao lakini muziki kidogo umepungua nguvu.”

”Ninaimani kwa sababu ya tuzo za Tanzania zilikuwa zinawahamasisha sana watu, wasanii walikuwa wakifanya kazi vizuri na kwa bidii anaamini kwamba siku moja ataitwa na atapewa heshima unajua tuzo ni heshima tu.”

”Kwa hivyo changamoto kidogo imepungua, kasi imepungua ni kutokana na tuzo kwa vijana maana mtu anaweza kujitungia nyimbo yoyote ambayo haina kichwa wala miguu sababu hategemei chochote lakini pia kampuni yangu ya Mo Faya inamipango hiyo ya kuwahamasisha vijana kufanya tuzo baadae Insha allah.”

Mwanamuziki huyo anayefanya vizuri barani Afrika amesema kuwa wasanii anao wakubali kutoka katika bara hili ni Oliver Mtukudzi kutoka Zimbabwe na mama Yvonne Chaka Chaka wa Afrika Kusini.

Related Articles

106 Comments

  1. Yaan Mziki wa siku hizi umekuwa fujoo..Mtu hakai kidogo akajipanga akaimba kitu kinchaoleweka badala yake amekurupuka na kutoa nyimbo kisa amfikie Fulan…Hii inachangia kuporomoka kwa radha ya Music…Nataman wale wasanii wa Zaman km kina Chid Benz Dully Embi Dog warudi kurejesha heshma ya Tansina yenu

  2. Ni kwel ukisemacho #kingKIBA now adays mziki wa bongo fleva umeshuka sana si kitambo kile japp wanajarbu ku umodifie kwa biti mbali mbali lakin wap. Wanaoharibu mziki huu ni wadau pia wa muzki, hasa ma underground producers sitowataja majina ila hawa madogo wana kopi sana beats na kusample biti za mbele yan kama “trap” beats sio asili yetu na cha ajabu hawafiki mbali. Mm naweza sema hata ma producers fake wanaharibu mziki utakuta anagonga biti zake chumban na kuanza kujiita producer, beats nyimbo znapgwa leo badae inakua kama big G yan…no flava sahv ni upuuz tu.

  3. Yan wew unaongea hivyo wakati dunian mziki unaopendwa ni trap ?na wasanii kibao wanaimba trap kama migos from america na wanakubalika,mim nawapongeza wasanii wa saivi kwasababu wanaendana na soko na ndo mana mzk upo kimataifa zaid sio kama zaman mzki unaishia east africa

  4. Frank Keyce wewe trap sio mziki wako kama asili yako japo tunaenda kwa utandawazi kwa sawa lkn kumbka ata hao wanapndasikilizaladha mpya sio una kop kop flava sawa…..ushawai ona wahindi wanafanya trap unaosema unakubalika kidunia na dunia ya nan??unaongea nini ndgu una jua mana ya originality flava ww

  5. We kama ni asili mbona jlo ameamua kutoa wimbo wa kiispaniola wakati sio asili yake ? Sababu ni kwamba aliona mziki unaouza sana ni wa kispaniola ndo mana kafanya hivyo ,kwahyo jamaa angu usikariri asili wew angalia mziki unampa nin msanii baada ya kuimba

  6. 🤰
    ___________________
    usihangaike tena na tiba
    Isiyorafiki kwa tatizo lako
    la;
    .
    #KUTOKA_UCHAFU_UKENI
    #HARUFU_MBAYA_UKENI
    #MIMBA_KUHARIBIKA
    #UVIMBE_TUMBONI
    #MIWASHO_UKENI
    #KUKOSA_MTOTO
    #FANGUS_SUGU
    #U.T.I_SUGU
    #P.I.D
    __________________
    Tiba zetu zote ni asilia.
    Tumehudumia wat wengi,
    na wameshapona kabisa.
    .
    Follow page yetu ya tiba
    @uti_pid_fangus_uzazi
    @uti_pid_fangus_uzazi
    __________________
    .
    Piga #0746774055

  7. sikweli, mziki ndio umekua, kwa mara ya kwanza tunapitwa na nigeria ktk afrika na tunaongoza afrika mashariki ndio maana nchi kama madagascar pamoja na kuongea kifaransa bado wanajaa uwanjan kuckiliza mziki na hakuna kipindi ambacho mziki umepanda juu kama mda huu

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents