Alikiba, Diamond, Joh Makini, Fid Q, Harmonize, Young Dee, Dogo Janja wapitiwa na ‘panga’ la Edu Boy

Msanii wa muziki Bongo, Edu Boy ameamua kujilipua katika ngoma yake mpya ‘Tunasafisha’ kwa kuwachana wasanii kibao wa Bongo Flava.

Katika ngoma hiyo ambayo Edu Boy amewashirikisha Amber Lulu na Belle 9 amewachana wasanii kama Alikiba, Diamond, Joh Makini, Fid Q, Harmonize, Young Dee, Dogo Janja, Ommy Dimpoz na wengineo.

Rapper huyo kutoka Rock City katika verse ya kwanza amejaribu kuficha majina ya Diamond na Alikiba kwa kuwataja wanyama kama Simba na Tembo lakini ni wazi amewalenga wao kutokana na kuwa na historia na majina yao.

Hii ni baadhi ya mistari inayopatikana katika ngoma hiyo.

Simba wa sasa hana madhara sana, labda Tembo kwa Dimpoz kupambana jipange sana/

Sina beef moyoni nina kitu, Joh katoa ngoma na Davido ka hakijatokea kitu/

Classic sound ukinisikia kwa radio, eti Bongo Bahati mbaya wakati unaishi studio/

Edu Boy na Mwanza Mwanza damu damu, kinachompoteza Baraka siyo kipaji ni nidhamu/

Namkubali sana Jux kwa sauti ya Saigoni, hiyo mivimbo ya Harmo je angekuwa Diamond/

Tusingepumua kwa hizo sifa, pale Wasafi nahisi angebaki Nillan na Tiffah/

Kwa viben ten Wolper anaongoza, ila kwa unafiki Dogo Janja namba moja/

Game noma mpaka Fid amesema-shake, ashukuru remix isingekuwa fresh/

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW