Burudani

Alikiba kaiba Cinderella?

AlikibaHivi karibuni kumezuka mgogoro mkubwa kiasi cha kufikia hatua ya kupelekana mahakamani baada ya msanii asiyejulikana kuibuka na kudai kaibiwa wimbo wa “Cinderella”ulioimbwa na Alikiba.

Alikiba

 

Hivi karibuni kumezuka mgogoro mkubwa kiasi cha kufikia hatua ya kupelekana mahakamani baada ya msanii asiyejulikana kuibuka na kudai kaibiwa wimbo wa “Cinderella”ulioimbwa na Alikiba.

 

Bongo5 lilimtafuta Alikiba ili aweke mambo wazi kuhusiana na shutuma hizo, na alisema “Nilishituka sana kuona kwenye magazeti yakiandika eti mimi nimemdhulumu huyu mtuwimbo huu wa ‘Cinderella’, pia akidai hapo zamani nilikuwa nafanya nae mazoezi, kwa kweli hizo ni fitina tu kwani mimi huu wimbo nimeutunga mwenyewe nyumbani, nikiwa na wadogo zangu na walikuwa wanaupenda sana na nimetunga muda mrefu hata kabla sijajulikana. Sasa iweje leo niambiwe nimeiba wimbo na hata huyu mtu mwenyewe simfahamu, ila sina wasi wasi ushaidi wote ninao nasubiri tu hiyo siku ya kwenda kwa Pilato” Alikiba.

 

Alikiba ameweza kujizolea umaarufu mkubwa kupitia wimbo wa “Cinderella” mwaka huu japokuwa alianza rasmi kujishughulisha na masuala ya muziki tangu mwaka 2004, aliposhirikishwa kwenye wimbowa msanii Abby Skills uliojulikana kwa jina la “Maria”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents