Promotion

Alikiba kupiga kazi Marekani

Ali Kiba Seven ndani ya One8 Press

 

Mwanamuziki mkali wa Kitanzania Ali Kiba anatarajiwa kwenda Chicago nchini Marekani kuungana na wanamuziki wengine maarufu wa Afrika akiwemo Amani (Kenya), Navio (Uganda), Fally Ipupa (RDC), 2 Face (Nigeria), JK (Zambia), 4×4 (Ghana) na Movaizhaleine (Gabon), kuunda kundi bora la muziki la Afrika linalojulikana kama ONE8 linalojiandaa kurekodi na mwanamuziki maarufu wa R&B Duniani.

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwa wanamuziki wa Afrika kuungana kama ilivyotokea hivi.Ushirikiano huu wa nyimbo pamoja na Video umeonyesha ushirikiano mzuri wa Afrika na Nchi za Nje. Kundi la ONE8 ndiyo mshiriki mkuu katika mpango huu na wanashirikiana kwa karibu zaidi na kwa usawa na mwanamuziki bora wa R &B wa marekani mwenye makazi yake jijini Chicago akiwa na timu yake ambao wamefurahishwa sana kufanya kazi na wasaanii hawa kutoka Afrika.

Japokuwa Ali Kiba alitoa Albam yake ya kwanza mwaka 2008 amefanikiwa kuwa mmoja wa wanamuziki bora barani Afrika, albam yake ya kwanza ilipata mafanikio makubwa Afrika mashariki kwa kuwa ndio albam iliyoongoza kwa mauzo katika ukanda huu.

Ali Kiba anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika kundi la ONE8. Wakati wanamuziki wote 8 kutoka Afrika wakiondoka kwenda nchini Marekani, mashabiki wa muziki duniani kote wataunganishwa nao kupitia mitandao mbalimbali kama vile Facebook, Twitter, Flicker na Youtube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents