Michezo

Alikiba kwa mara ya kwanza kushuka dimbani kuikabili KMC, kocha adai anaweza funga zaidi ya mabao 25

Mwanamuziki wa Bongo na mshambuliaji wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Alikiba leo anatarajiwa kushuka kwenye dimba la Mkwakwani jijini kuanza kibarua chake rasmi cha kuitumikia timu hiyo kwenye mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya KMC.

Coastal ambayo imefanya vizuri kwenye michezo yake iliyo pita ya mwanzo mwa msimu wa ligi itamtumia Alikiba kwenye safu ya ushambuliaji huku wakiamini kuwa msanii huyo aliyeamua kukitumikia kipaji chake cha soka atafanya vizuri.

Video: Alikiba aishushia neema Coastal Union ‘nimekuwa mdhamini mkuu kupitia kinywaji changu cha Mo Faya’

Katika mahojiano yake kocha wa klabu ya Coastal Union, Juma Mgunda amedai kuwa Alikiba ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo hata wakufunga mabao 25 msimu huu.

“Mashabiki wa Coastal Union wa­nachotakiwa kufahamu ni kwamba timu hii imesajili wachezaji 30 na kila mchezaji anataka kucheza, hivyo muda ukifika kila mmoja ataonekana uwanjani.

“Najua wengi wanamuulizia Alikiba, niseme tu ataonekana uwanjani muda si mrefu na niwaambie ni mshambulia­ji mzuri na anaweza kufunga zaidi ya mabao 25 msimu huu,” alisema Mgun­da.

Mbali na uchezaji wake, Alikiba pia amewadhamini wagosi hao wa kaya Coastal Union msimu huu mwaka 2018/19 ambao mpaka sasa maendeleo yao si haba baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mmoja na kushika nafasi ya nne kwa alama zao nne juu ya mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wenye pointi sita na michezo miwili.

Related Articles

11 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents