Burudani

Alikiba yupo kwenye mchakato wa kuachia ngoma – Abdu Kiba

Msanii wa Bongo Flava, Abdu Kiba amedai kwa sasa Alikiba yupo katika mchakato wa kuachia ngoma mpya.

Muimbaji huyo ambaye ni ndugu na Alikiba na chini ya Kiba Squared walishatoa hit song kama Kidebe, amesema Alikiba kwa sasa yupo nje ya nchi na akirejea ngoma mpya itadondoka.

“Alikiba kwa sasa yupo nchini Kenya amekwenda kufanya jambo na gavana wa Mombasa Joho ila nadhani hawezi kumaliza wiki atarudi nchini, kwa hiyo nachojua mimi yeye yupo kwenye mchakato wa kuachia ngoma mpya hivyo naamini akisharudi kila kitu kitakuwa sawa,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.

Alikiba kwa sasa ana muda wa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoe wimbo wa Aje uliotoka May 19 mwaka jana kitu ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na mashabiki wake.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents