Burudani

Alikiba, Yvonne Chaka Chaka kuitikisa Dar kwa burudani

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ametangaza siku mbili tofauti tofauti za show yake ya funga mwaka kwa wakazi wa Dar Es Salaam.

Image result for yvonne chaka na alikiba
Yvonne Chaka Chaka na Alikiba

Alikiba kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, amesema kuwa show yake ya kwanza itafika Desemba 22, 2018 katika ukumbi wa Serena Hoteli.

Show hiyo Alikiba atasindikizwa na msanii mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka.

Show yake ya pili ambayo itakuwa fungwa mwaka itafanyika Next Door tarehe 29 Desemba 2018.

2. 1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es salaam 22 . December. 2018 2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018.

Alikiba na Yvonne Chaka Chaka walishawahi kurekodi wimbo lipindi cha nyuma, lakini hadi sasa wimbo huo haujatoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents