Shinda na SIM Account

Aliyefanya jaribio la kuiba mwenge wa Olimpiki Brazil atiwa mbaroni

Polisi nchini Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.
t04_20908853

Video kuhusiana na tukio hilo, inamuonyesha mtu huyo akipigwa mieleka na walinda usalama, baada ya kuingia katika msafara wa watu na kuelekea moja kwa moja hadi kwa mtu aliyekuwa na mwenge huyo akiwa na nia ya kumpokonya.

Mtu huyu alinaswa na kuchukuliwa, huku mbio za mamani za mwenge huo zikiendelea muda mfupi baadaye.

Mwenge huo unatazamiwa kufika mjini Rio de Janeiro tarehe 4 mwezi ujao, kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano ya Olimpiki.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW