Habari

Aliyefanyiwa operesheni ya kichwa apata nafuu

HALI ya mgonjwa Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), inaendelea vizuri.

Na Mwandishi wa Mwananchi


HALI ya mgonjwa Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), inaendelea vizuri.


Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili jana jioni kwa njia ya simu, kaka wa Didas, Sestis Marishay alisema ndugu yake anaendelea kuapata nafuu kidogo ukilinganisha na hali aliyokuwa nayo hapo awali.


Alisema hivi sasa hapumui kwa kwakutumia mipira na anaweza kutizama,kusikia akielezwa jambo.


Marishay alisema Didas ambaye alifikisha siku 10 jana akiwa kwenye chumba cha uangalizi maalum wa madaktari (ICU) tangu alipofanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu, wanamshukuru Mungu kwani hata hatua hiyo aliyoifikia hawakuitegemea.


�Ninamshuru Mungu kwani hata hapo alipofikia hatukutegea kama angefika kwa sasa anaweza kupumua bila kutumia mashine pia anaweza kuelewa ukimwambia jambo anafanya japokuwa hajawa na uwezo wa kuzungumza lakini tunamatumanini,�alisema Marishay.


Kuhusu Mgaya pia taarifa zilizolifikia gazeti hili jioni kutoka kwa mwanafamilia wakaribu kwa masharti ya kutotajwa gazetini, zinaeleza kwamba anaendelea vizuri japo kuwa tatizo la kichwa bado lipo linaendelea kumsumbua.


�Jeraha lake linaendelea vizuri japokuwa tatizo lake bado lipo,� alisema.


Novemba mosi mwaka huu wagonjwa hao Emanueli Didas na Emanuel Mgaya walifanyiwa upasuaji kinyume na matatizo yao ambapo Didas alitakiwa afanyiwe upasuaji wa mguu baada ya kupata ajali ya pikipiki badala yake akafanyiwa upasuaji wa Kichwa .


Na mgojwa mwingine ni Mgaya aliyetakiwa kufanyiwa uapasuaji wa kichwa kutokana na matatizo yaliyokuwa yakimsumbua naye alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya upasuaji wa kichwa.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents