Burudani

Aliyekuwa meneja wa Diamond, Papa Misifa kumrudisha Killy ‘huyu ni Simba mwingine’

Aliyekuwa meneja wa zamani wa Diamond, Papa Misifa amedai anajipanga kumrudisha msanii wa muziki Killy ambaye alifanya vizuri na wimbo ‘Rudi’ huku akidai msanii huyo ni Simba mwingine ndani muziki wa bongofleva.

Hii ni moja kati ya kazi za msanii huyo.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii Mkurugenzi msaidizi wa label ya Al Jazeera Entertainment, Meneja Kesy amedai msanii huyo anakuja kivingine ili kufanya mapinduzi makubwa katika muziki wa bongofleva.

“Al Jazeera Entertainment tayari ina mchango mkubwa katika muziki huu kwa sababu kuna wasanii wakubwa wengi ambao wanafanya vizuri katika muziki na wamepita katika mikono ya Al Jazeera, Kwa hiyo ninavyosema anakuja Simba mwingine namaanisha anakuja kufanya mapinduzi katika muziki kwa sababu yeye ni zaidi ya hawa Simba ambao wapo mtaani,” alisema meneja huyo.

Aliongeza, “Najua muziki unachangamoto nyingi lakini kwa sasa hatutaki kufeli kwa sababu huyu msanii tunaujua uwezo wake, ni msanii ambaye ana uwezo mkubwa kuliko hata wasanii wengi ambao wanasikika na kama nilivyosema huyu msanii nilimpata kwa Maneky, kwahiyo ni msanii ambaye anaweza kufanya chochote kikawashangaza watu ndani ya muziki,”

Kwa upande wa muimbaji huyo ambaye alikuwa kimya, amedai bado anaona ana nafasi ya kufanya zaidi katika muziki huyo.

“Kwanza nianze kuwashukuru Watanzania wote kwa kunipokea vizuri na wimbo wangu ‘Rudi’ na video yake ilitengenezwa na Nisher. Ile ni kazi ambayo iliweza kunifungulia njia, lakini kuna mengi mazuri ambayo hayakupata nafasi na huu ndio wakati wake. Simba mwingine nakuja na wimbo ‘Nikwambie’.

“Ni wimbo mkali sana ambao utakuja kufanya vizuri. Pia video nimefanya Adam Juma na imegharimu zaidi ya milioni kumi. Kwa hiyo naweza kusema itakuwa ni moja kati ya ngoma kali za mwaka huu,”

Kuhusu suala la kujiita ‘Simba mwingine’ muimbaji huyo alidai anatumia aka hiyo ili kuonyesha yeye ni mkali zaidi ya wasanii hao ambao wanajumia jina ilo kudhihirisha ukali wao katika muziki.

“Sio nia yangu kujigamba lakini Simba ni jina ambalo linatumika na wasanii kuonyesha ukali wao, ndiyo maana nikasema mimi sio Simba wakaida mimi ni Simba mwingine mla nyama kimya kimya,”

Muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya wimbo wake mpya ambao utatoka katika siku za usoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents