Burudani

Aliyekuwa mpenzi wa mtoto wa Whitney Houston afikishwa mahakamani

Nick Gordon ambaye alihusishwa katika kusababisha kifo cha mtoto wa mwanamuziki Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown amefikishwa mahakamani kwa kumpiga mpenzi wake.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na polisi, Nick alikamatwa Jumamosi iliyopita kwa kosa la kumpiga na kumteka mpenzi wake mpya kutokana na kipigo alichompa mrembo huyo siku ya Ijumaa ambacho kimempelekea mpaka kulazwa hospitalini.

Hata hivyo Nick ametakiwa kulipa faini ya dola 15,000 mkosa la kumteka mpenzi wake na dola 500 kwa kufanya unyanyasaji huo hadharani.Chanzo cha karibu kimeeleza kuwa Nick hana hizo pesa kwa kuweza kujikwamua katika sakata hilo ila anaweza kuachiwa wakati wowote.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents