Habari

Aliyekuwa mshauri wa Usalama John Bolton: Rais Donald Trump alitaka kuongoza zaidi ya mihula yake miwili

Urais wa Donald Trump tayari umeweka orodha ndefu ya vitabu, lakini kitabu cha hivi karibuni cha aliyekuwa mshauri wa usalama kitaifa , John Bolton kimevutia watu wengi, na hii ni kutokana na wadhifa aliokuwa nao mwandishi.

Kazi yake – Chumba ambacho jambo hilo lilitokea – kinaonyesha taswira ya rais kutojua ukweli wa masuala ya mazingira na siasa na nia yake kuu ni kutamani kuchaguliwa kwa mara nyingine.

Kukosolewa kwa bwana Trump kumesababisha watu kuhoji ni kwa nini bwana Bolton hakuzungumza hayo wakati wa kusikilizwa kwa madai dhidi ya rais wakati rais mwenyewe aliwaita washauri wakuu wa zamani wa ulinzi kuwa- hawajui wajibu wao na wazee ambao hawana akili.

Ikulu ya rais Marekani ilikuwa inajarbu kuzuia kitabu kisitoke, lakini vyombo vya habari vya Marekani vilikuwa na nakala ambayo vilianza kuichapisha.

Baadhi ya madai ambayo yalivutia wengi katika kitabu hicho ni haya:

1. Trump alikuwa anataka msaada kutoka China ili kushinda uchaguzi kwa mara nyingine…

Katika kitabu hicho, bwana Bolton alielezea kuhusu mkutano kati ya rais Trump na mwenzake wa China bwana Xi Jinping katika kikao cha mataifa yenye nguvu ya G20 ambacho kilifanyika mwaka jana nchini Japan.

Rais wa Marekani “alichukua fursa hiyo na kubadili majadiliano kwa kuongelea uchaguzi wa rais unaokuja mwaka huu (2020],akitaja uwezo wa uchumi ,wa China na kumsisitiza Xi kuhakikisha kuwa anashinda,” bwana Bolton aliandika.

“Alifafanua kuhusu umuhimu wa wakulima na kuongezeka kwa manunuzi ya maharage ya soya na unga wa ngano baada ya uchaguzi wa Marekani.”

Kilimo ni sekta kubwa katikati ya magharibi mwa mataifa ya Amerika kusini ambayo yalimsaidia vyema bwana Trump kushinda uchaguzi wa mwaka 2016.

2. … na alisema kujenga kambi za magereza ndio jambo sahihi kufanya’

Jinsi China inavyowafanyia Uighurs na jamii nyingine za watu wachache kumeleta malalamiko ya kimataifa ,ikiwa watu wapatao milioni walidhani kuwa watashikiliwa katika kambi zilizoko ukanda wa Xinjiang.

Siku ya Jumatano, rais Trump alitoa idhini ya kuunga mkono maafisa wa China ambao walikuwa wanahusika kuwafunga watu wengi na hiyo ikachochea China kukasirishwa na jambo hilo.

Donald Trump na Xi Jinping katika picha nchini Japanrais Trump amemsifu rais wa China Xi Jinping huku akikabiliana nanaye katika vita vya kibiashara

Lakini kitabu cha bwana Bolton kinaeleza kuwa wakati bwana Xi akitetea kujengwa kwa kambi , rais wa Marekani alitoa idhini kwa China kuendelea na hatua hiyo.

“Kwa mujibu wa mkalimani wetu ,” bwana Bolton aliandika, “Trump alisema kuwa Xi aendelee na ujenzi wa kambi , jambo ambalo Trump alidhani kuwa ni jambo sahihi kulifanya.”

3. Trump alitoa hongo kwa madikteta’

Bwana Trump aliridhia kuingilia utafiti wa uhalifu na hata kutoa hongo kwa madikteta ambao aliwapenda,” bwana Bolton aliandika.

Kwa mujibu wa kitabu hicho, bwana Trump alitoa msaada kwa rais wa Uturuki bwana Recep Tayyip Erdogan mwaka 2018 kufanya uchunguzi katika kiwanda cha Uturuki kuhusu madai ya ukiukwaji wa vikwazo vya Iran.

Rais wa Marekani alisema kuwa alikubali kushughulikia vitu ambavyo waendesha mashtaka waliohusika ni watu wa Obama.

4. Democrats kufungua madai dhidi ya rais

Katika kitabu hicho, bwana Bolton aliunga mkono madai ya Democrats kuwa rais Trump alikuwa anataka kuondoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine ili kuisukuma serikali kumchunguza mpinzani wake Joe Biden. Madai hayo dhidi ya rais yalipelekea rais Trump kushtakiwa.

Hata hivyo bwana Bolton alikikosoa chama cha Democrats katika kitabu chake, kwa kusema kuwa walikuwa wakilenga upande mmoja wa madai dhidi ya rais katika suala la Ukraine peke yake.

Alisema kama wangeongeza wigo wa uchunguzi basi Wamarekani wengi wangefahamu kuwa rais Trump amefanya uhalifu mkubwa sana na ilikuwa ni muhimu kuondolewa madarakani.

 

Aidha bwana Bolton hajasema iwapo madai hayo mapya anayotoa yanaweza kumuondoa rais madarakani.

Alikataa kutoa ushahidi wakati madai dhidi ya rais yakisikilizwa mwaka jana na baadae alizuiliwa kuwasili bungeni na chama cha Republicans.

5. Trump alitaka kuhudumu zaidi ya mihula miwili

Bwana Bolton alisema bwana Trump alimwambia kiongozi wa China kuwa Marekani iko tayari kumsaidia kubadilisha katiba ili aweze kutawala zaidi ya mihula miwili.

“Jambo la kushangaza ni pale bwana Xi aliposema kuwa anataka kufanya kazi pamoja na Trump kwa zaidi ya miaka sita na Trump alijibu kuwa katiba inaweka mwisho wa mihula miwili tu .

“Xi alisema Marekani ina uchaguzi mara nyingi sana , kwa sababu alikuwa hataki kuacha kufanya kazi na Trump ambaye alionekana kukubaliana naye”.

6. Trump hakufahamu kuwa Uingereza ina silaha za nuklia…

Uingereza ni taifa la tatu baada ya Marekani na Urusi kujaribu silaha za atomiki mwaka 1952. Lakini Uingereza ni sehemu ya klabu ndogo za mataifa ambayo yana silaha za nuklia lakini jambo likaonekana kuwa geni kwa rais Trump.

Katika mkutano wa mwaka 2018 , na aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, bi.Theresa May aliitaja Uingereza kuwa taifa la nuklia.

Bwana Trump alijibu : “Oh, kwani na nyinyi mna nguvu za nuklia?”

Bwana Bolton alisema, “alijibu kwa kudhamiria na sio kwamba alikuwa anatania”.

7. … au kama Finland ilikuwa sehemu ya Urusi

Bwana Bolton alisema rais Trump alikuwa hana ufahamu wa mambo mengi.

Kabla ya mkutano na rais wa Urusi bwana Vladimir Putin katika mji mkuu wa Helsinki, aliuliza kama Finland ilikuwa ni sehemu ya Urusi.

Donald Trump na Vladimir Putin wakiamkuanaPresident Trump alikutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Helsinki

Kwa mujibu wa bwana Bolton aliona watu wake wa intelijensia walikuwa hawafanyi kazi yao ipasavyo kwa kumpa taarifa sahihi

8. Alikuwa karibu kujitoa Nato

Rais Trump alikuwa anasisitiza kulikosoa jeshi la Nato na kuita wanachama wengine kuongeza matumizi yao.

Pamoja na hayo Marekani ilibakia kuwa mwanachama, lakini bwana Bolton alisema katika mkutano wa Nato wa mwaka 2018 kuwa anataka kujitoa.

“Tutaondoka na hatutawatetea wale ambao hawajalipa,” alisema rais kwa mujibu wa bwana Bolton.

9. Kuivamia Venezuela ni jambo zuri

Sera moja kwa mataifa ya kigeni katika utawala wake Trump ambayo imekuwa ikimuuma kichwa kiongozi huyo ni taifa la Venezuela, ambapo Marekani imekuwa ikimpinga rais Nicolás Maduro.

Katika mazungumzo ya jambo hilo rais Trump alisema itakuwa vyema kuivamia Venezuela, na taifa hilo la Amerika ya kusini ni sehemu ya Marekani kiuhalisia.

Bwana Bolton aliandika mwezi Mei 2019 kuwa mazungumzo ya simu ya rais wa Urusi Vladimir Putin yaliondoa propaganada za ‘Soviet’ na kuhusisha na kiongozi wa upinzani nchini Venezuela bwana Juan Guaidó, katika wagombea wa urais wa 2016 Democratic Hillary Clinton, ambaye alikuwa anapambana karibu na Trump”.

Bwana Putin’alimkinga mshirika wake rais Maduro, bwana Bolton aliandika. Mwaka 2018, bwan Trump alimuita bwan Maduro kuwa dikteta ambaye alisalia madarakani licha ya vikwazo.

Katika mahojiano na ABC News bwana Bolton alisema bwana Trump: “Nadhani Putin anadhani anaweza kunitapeli.”

10. Hata washirika wake huwa hawakubaliani na maamuzi yake

Kitabu cha bwana Bolton kina mifano ya jinsi maafisa wa Ikulu ya Marekani wanavyombeza rais Trump.

Anaelezea kuhusu ikulu ya Whitehouse ilioshindwa na kazi , Ikulu ambayo mikutano inafananishwa na watu wanaopigania chakula badala ya juhudi za kuunda sera.

Wakati alipowasili Ikulu , mkuu wa maofisa bwana John Kelly alimpa tahadhari, “Hii ni sehemu mbaya ya kufanya kazi lakini utajua tu “.

Hata waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo, ambaye anaonekana kuwa ni mtu wake wa karibu anamuelezea Trump kuwa mtu mwenye majanga mengi.

Chanzo BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents