Tupo Nawe

Aliyekuwa rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey Nyange ‘Kaburu’ mambo safi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.

Image result for Aveva na Kaburu bongo5
Dhamana hiyo ni kuwa na Wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Tsh. Million 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 8 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo washitakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wamerudishwa mahabusu ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zachariah Hans Pope.

Image result for Aveva na Kaburu bongo5

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema jukumu la kuthibitisha shitaka kwa washitakiwa ni la upande wa mashitaka, pia kwa kosa mojamoja na sio kwa kutegemeana.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW