Habari

Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ashtakiwa kwa makosa haya

Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ameshtakiwa kwa makosa ya rushwa. Mashtaka yanahusiana na sheria zinazohusu “utajiri haramu na maagizo ya dharura “,imesema ofisi ya mwendesha mashtaka, ambayo haikutoa taarifa zaidi.

Image result for omar al-bashir

Jeshi lilimuondoa madarakani rais huyo wa muda mrefu mwezi April kufuatia miezi ya maandamano dhidi yake. Msemaji wa jeshi aliesma Alhamisi kuwa makosa yalifanyika wakati majeneraliwalipoamrisha kumalizika kwa mgomo wa kukaa mbele ya makao makuu ya jeshi ambapo waandamanaji wanadai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo.

Ghasia za mwezi Juni zilisababisha vifo vya watu 61, kwa mujibu wa maafisa, au 118,kwa mujibu wa madaktari wanaounga mkono waandamanaji wanaodai demokrasia.

Mazungumzo baina ya waandamanaji na baraza la kijeshi la mpito yalivunjika baada ya ghasia. Viongozi wa maandamano baadae waliyaita maandamano kuwa ni ukaidi wa raia , ambayo walisema hayana budi kukoma ili kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani.

Baada ya mkutano baina ya Tibor Nagy, Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan,jeshi lilisema kuwa lina matumaini Marekani inaweza “kuwa na mchango mzuri”.

Bwana Bashir alipinduliwa na kukamatwa tarehe 11 Aprili baada ya miongo mitatuya utawala wa kiimla nchini Sudan. Hajawahi kuonekana kwa umma tangu alipokamatwa.

Mwezi Mei alishtakiwa kwa makosa ya kuchochea nana kuhusika na mauaji ya waandamanaji. Mashtaka hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa kuhusu kifo cha ddaktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliyosababisha kumalizika kwa utawala wake mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Hatma ya Bwana Bashir haijawa wazi. Aliripotiwa kutiwa nguvuni mara baada ya kupinduliwa. Mnamo mwezi Disemba, waandamanaji walianza maandamanano dhidi ya uamuzi wa serikali wa kupandisha mara tatu kwa bei ya mkate.

Maandamano hayo ghafla yalibadilika kuwa hasira iliyosambaa kote nchini dhidi ya kiongozi huyo ambaye alikuwa mamlakani kwa miaka 30, yakiongozwa na madaktari.

Maandamano yalifanyika kwa wiki tano na shahidi mmoja anasema tarehe 17 Januari, vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waandamanaji na kumuua daktari.Waandamanaji walimshinikiza rais Omar Al-Bashir kuachia madaraka

Waandamanaji walimshinikiza rais Omar Al-Bashir kuachia madaraka

Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir uligubikwa na mapigano. Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika zama hizo hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.

Japo serikali yake ilitia saini makubaliano ya kumaliza vita mwaka 2005, vita vingine vilizuka tena – katika eneo la magharibi mwa Darfur.

Bw. Bashir alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo hilo.

Licha ya ICC kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake, ameshinda uchaguzi mara mbili mwaka 2010 na 2015, japo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi uliyopelekea ushindi wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents