Habari

Aliyelimwa kadi nyekundu kwa kupumua mbele ya mwamuzi, azungumza

Adam Lindin Ljungkvist, anayeichezea Pershagens SK, alikuwa uwanjani katika mchezo dhidi ya kikosi cha akiba cha Jarna SK kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Saba, Sweden.
red-card
Mchezaji wa Sweden ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi kumtuhumu kuwa alifanya vitendo visivyokuwa vya ‘kiungwana’ na ‘kiuanamichezo’ uwanjani.

Adam Lindin Ljungkvist, anayeichezea Pershagens SK, alikuwa uwanjani katika mchezo dhidi ya kikosi cha akiba cha Jarna SK kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Saba, Sweden.

Hata hivyo, beki huyo wa kushoto alionyeshwa kadi ya pili ya njano iliyomtoa uwanjani dakika ya 93, baada ya kupumua akiwa karibu na mwamuzi.

“Nilikuwa na mchafuko wa tumbo, hivyo nikajikuta nimeshaponyokwa,” alisema nyota huyo wa miaka 25 alipozungumza na Lanstidningen Sodertalje.

“Nilimuuliza mwamuzi, ‘hivi, siruhusiwi kupumua hata nikiwa nimebanwa?’ ‘Hapana,’ alinijibu “Sikuelewa, lakini labda alidhani nilifanya hivyo mkononi na kumrushia puani. Lakini sikufanya hivyo.”

“Nilizungumza na mwamuzi na nikamwambia sikufanya makusudi bali ilikuwa ni mchafuko wa tumbo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents