Bizzare

Aliyempa mimba mke wa mtu aomba msamaha kwa kumnunulia mumewe gari la kifahari

Mwanamme mmoja mwenye asili ya Nigeria imemlazimu kumkabidhi mwanaume mwenzie gari la kifahari kama kipozeo baada ya kumpa ujauzito mke wa mwenzie.

Gari alilopewa baada ya mkewe kupewa ujauzito aina ya Mercedes-Benz (G-Glass 2017)

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina moja la John ambaye makazi yake yapo nchini Afrika Kusini alimpa mimba mke wa mtu pasipo kujua.

John amesema alikutana na mwanamke huyo Mgahawani jijini Johannesburg, na ndipo alipomtongoza na kumkubalia.

Mwanaume huyo amesema kabla ya kumtongoza alimuuliza mwanamke huyo kama ameolewa lakini alikataa katu katu kuwa hajaolewa.

John ameongeza kuwa baada ya kudumu nae kwenye mahusiano kwa muda wa miezi mitano, mwanamke huyo alimwambia kuwa anaujauzito wake na kumueleza ukweli kuwa ameolewa ila alimdanganya ili apate pesa.

Najua nilichokifanya ni kibaya lakini nafurahi kuwa mumewe amepokea zawadi yangu. Alikubali kuwa mkewe ni mjamzito na ujauzito ni wangu na uzuri ni kwamba atazaa mtoto wangu. Nashukuru Mungu kwani wakati naenda kutoa taarifa mumewe alikuwa mwenye jaziba lakini nilipompelekea gari alionesha tabasamu na kunikumbatia. Najua nimemkosea lakini mkewe alikuwa na makosa zaidi angeniambia ukweli nisingelikubali kufanya nae mapenzi.“Amesema John kwenye mahojiano yake na gazeti la Daily Live la nchini Afrika Kusini.

Mmiliki wa Mgahawa huo ambaye ndiye muajili wa Mwanamke huyo amesema alijua kuwa mwanamke huyo alikuwa kwenye mahusiano na John lakini hakufikiria kama wangefikia hatua ya kupeana mimba, huku akilaani tukio la mumewe kukubali kupokea gari.

John alimpa zawadi ya gari aina ya Mercedes-Benz (G-class) 2017 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 270 za kitanzania.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa majirani wa Mwanaume huyo mwenye mke aliyepewa ujauzito. Wamesema mwanaume huyo anafanya kazi migodini na huwa anakaa huko kwa muda mrefu.

Kwa upande mwingine tayari John ameafikiana na Mwanaume huyo kumtunza mkewe mpaka atakapojifungua na kukabidhiwa mwanaye.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents