Michezo

Aliyempiga McGregor yupo tayari kuzipiga na ‘Money’ Mayweather, pambano kufanyika Moscow

Bingwa wa UFC, Khabib Nurmagomedov amesema kuwa yupo tayari kupigana na mwanamasumbwi Floyd Mayweather huku akihitaji pambano hilo lifanyike jijini Moscow.

Bingwa wa UFC raia wa Urusi, Khabib Nurmagomedov

Nurmagomedov raia wa Urusi ni mpiganaji anayetumia ‘martial artist’ anahitaji kupigana na Mayweather ambaye tayari alishampiga Conor McGregor katika pambano lililoingiza mkwanja mrefu.

Mpiganaji huyo anayegonga vichwa vya habari toka apate ushindi nbaada ya kumpiga McGregor jijini Las Vegas Oktoba 7 mwaka huu raundi ya nne, alipoulizwa kama yupo tayari kuzipiga na Mayweather amesema kuwa ni jambo linalowezekana.

https://www.instagram.com/p/BpRfHZ8n3SO/?utm_source=ig_embed

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Khabib Nurmagomedov ameandika kuwa amekutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo wa masumbwi nchini Urusi, Umar Kremlev kuzungumzia pambano lake dhidi ya Mayweather.

“Hii leo nimekutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo wa masumbwi nchini Urusi @umar_kremlev tumejadiliana kuhusu pambano la Mayweather,”

“Tunahitaji tupigane jijini Moscow katika eneo la ‘legendary Luzhniki arena’, hakika ni sehemu inayoweza kuchukua  watu 100,000 lakini pia itaweka historia katika kuuza haki za matangazo.”

“Na moja kati ya jambo muhimu ni kuwa baba yangu atakuwa pembeni yangu, wala hauitaji kibali kuja Moscow, swali kwa mashabiki zangu je mnaniamini au mnaamini atanishinda kwenye mchezo wa masumbwi ?.”

Bondia wa Marekani, Conor McGregor

Mrusi huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhitaji kupigana na ‘Money’ Mayweather mara baada ya kumpiga Conor McGregoout.

Mayweather ambaye alishatangaza kustaafu alirejea tena ulingoni na kumpiga McGregor mwaka 2017 na kuweka rekodi yake sawa ya kushinda jumla ya mapambano 50-0 bila kupigwa hata moja.

Kama pambano hilo litafanyika jijini Moscow kama Nurmagomedov alivyosema basi itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mayweather kupigana nje ya Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents