Shinda na SIM Account

Aliyemuua ndugu wa Rihanna afikishwa kwa pilato

Mwanaume mmoja amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji, Tavon Kaiseen Alleyne, 21 ambaye ni ndugu wa mwanamuziki wa kimataifa Rihanna.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Nation News zinasema, kijana huyo anafahamika kama Shawayne Dashawn Williams ana umri wa miaka 23, amefunguliwa mashtaka ya mauaji hayo ya Alleyne ambayo yametokea wiki iliyopita katika sikukuu ya Christmas.

Shawayne alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatano hii na kesi hiyo iliahirishwa na mtuhumiwa alirudishwa gerezani huku hukumu ya kesi hiyo ikipangwa kutolewa January 31 ya mwaka huu.


Picha ya Shawayne Dashawn (kushoto) akiwa amekamatwa na polisi

Kabla ya kutokea kwa tukio hilo la mauaji, marehemu Alleyne alikuwa akitembea karibu na nyumba yake majira ya 1 usiku kabla ya kufatwa na mtu asiyefahamika na kisha kumiminiwa risasi za kutosha. Hata hivyo Alleyne alikimbizwa hospitali ya Queen Elizabeth iliyopo Bridgetown lakini alifariki dunia.

Wakati huo huo marehemu Tavon Alleyne alikuwa na Rihanna saa moja kabla ya kufariki dunia wakisherehekea pamoja sikukuu ya Christmas.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW